Dunia katika nyakati na zama hizi imekuwa ya kidijiti, mambo mengi na shughuli nyingi zinafanyika kutegemea Mtandao. Uandishi wa habari wa kidigitali unazo faida nyingi.

Katika tasnia ya habari, mifumo na kanuni za uandishi ni zile zile lakini vifaa na teknolojia ndivyo ambavyo vinaenda vikibadilika siku hadi siku kulingana na mabadiliko ya kiulimwengu. Uandishi wa habari ni moja ya tasnia zenye mchango muhimu na wa pekee katika maendeleo ya jamii na mataifa ulimwenguni.

Zipo faida nyingi zitokanazo na kuwa Mwandishi wa kidigitali. Miongoni mwa hizo ni kama zifuatazo;

  • Humuwezesha na kumsaidia Mwandishi kujua na kuchagua mtandao sahihi wa kijamii wa kutumia kulingana na mahitaji ya rika na kundi husika (hadhira) husika. Kwa mfano masuala ya sasa, mtandao wa Twitter ndio unakaa utamfaa zaidi Mwandishi wa kidigitali anayeangazia masala ya kisiasa na hii itamfanya kazi yake kukua na kufikia idadi kubwa ya hadhira ambayo imejikita katika kufuatilia masala ya sasa.
  • Kufikia idadi kubwa ya wasomaji ndani ya muda mfupi. Kwa kutumia mitandao ya kijamii au tovuti, kwa mfano mtandao wa Facebook wenye watumiaji wasiopungua niliona tatu kwa mwezi. Mwandishi wa habari wa kidigitali anaweza kuandika habari yake na amafikia idadi kubwa ya wasomaji ndani na nje ya nchi ndani ya muda mfupi.
  • Kupunguza gharama; hii pia ni miongoni mwa faida za kuwa Mwandishi wa kidigitali kwani Mwandishi anaweza kutumia na kusambaza habari yake katika tovuti na mitandao ya kijamii zaidi ya mmoja kwa kutumia data ya intaneti ile ile ambayo anakuwa ameunganisha na kifaa kile kile yaweza kuwa simu janja au kompyuta mpakato haimlazimu kuwa na vifaa vya aina mbili tofauti ili kuweza kuwasilisha kazi yake kwa walaji wake.
  • Urahisi katika uchapishaji wa picha na video zenye ubora kwa kutumia mitandao ya kijamii na programu mbali mbali kama vile instagram, Snapchat, TikTok na hata canva katika kutengeneza na kuzalisha picha nzuri za matukio kwa ajili ya kuweka mkazo na kuboresha habari.
  • Kufahamu juu ya kinachotokea au kuendelea ulimwenguni kwa wakati. Mitandao ya kijamii hujulisha maelfu ya watumiaji juu ya kinachotokea ulimwenguni kwa wakati. Kwa kutumia simu au kompyuta na kufuatilia mashirika makubwa ya habari kwa mfano BBC, CNN na taasisi kubwa ulimwenguni Mwandishi anaweza kujua juu ya kinachoendelea ulimwenguni katika nyanja za kiuchumi, kisiasa, kijamii na hata matukio mbalimbali ndani ya muda mfupi.
  • Pia Humuwezesha Mwandishi kutoa taarifa na takwimu likizo za kweli kwa kuepusha kutoa machapisho yasiyo na uhakika kwa kuwa taarifa na tafiti nyingi zenye ukweli na uhakika zimepatikana na zipo katika tovuti mbalimbali mtandaoni.

Japo uandishi wa habari wa kidigitali una faida nyingi, lakini pia zipo changamoto mbalimbali zinazoikabili tathnia hii ikiwemo udukuzi wa taarifa na akaunti za waandishi, matatizo ya mtandao kutokuwa thabiti na wenye uhakika, pia upatikanaji wa data kwa gharama kubwa jambo ambalo linawakwamisha waandishi wengi kufanya vitu vikubwa kuendana na ulimwengu wa kidigitali.

Imeandaliwa na Jesca Beatus  | Maendeleo Development Foundation

Mwandishi wa Kidijitali 2021/22

Boresha Habari Project

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *