Ni kwa namna gani Matumizi ya kidigitali kwa wanahabari Tanzania yanakumbwa na changamoto nyingi Mpaka kupelekea wanahabari wengi kushindwa kuweka maudhui yao katika mitandao ya kijamii Na hivyo kushindwa kufikia soko la watumiaji wengi wa mitandao hiyo ambapo kwa sasa karibu ya asilimia kubwa ya walaji wanapatikana katika mitandao ya kijamii.

Baadhi ya wanahabari wengi nchini Tanzania hawana elimu pana juu ya mitandaoya kijamii katika matumizi sahii ya kuweza kutangaza kazi zao za kihabari hali hii inapelekea kwa wao kushindwa kutumia mitandao hiyo kwa kushindwa kuandaa maudhui sahii yakuendana na teknolojia ya sasa na kujikua wanaachwa na dunia ya sasaya kidigitali.

Ni kwa Namna gani ambavyo uandishi wa habari wa kidijitali unaweza kubadilisha maisha ya mwanahabari kwa ujumla

Malengo ni kuhakikisha wanahabari hasa wanawake Tanzania wanakuwa na mtazamo chanya juu ya uandishi wa habari kidigitali katika kutumia majukwaa ya mitandao ya kijamii katika kusambaza kazi maudhui yao lakini kujua matumizi sahii ya majukwaa yao na uwasilishaji mzuri wa maudhui yao ili kuweza kumfikia mlaji yaani mtumiaji wa mitandao hiyo

Lengo kuwapa elimu sahii wanahabari juu ya matumizi sahii ya mitandao hiyo yakihabari lakini pia kujua sheria za nchi ya Tanzania juu ya mitandao hiyo ya kidigitali

taasisi mbali mbali na mashirika yanayojihusisha na maswala ya kihabari kuandaa program za kuwafikia wanahabari wengi ili kuwapa elimu lakini kuwafadhili katika vifaa vya kufanyia kazi hizo kwani imekuwa changamoto kubwakwa wanahabari wengi kukosavifaa vya kielekroniki katika kazi kitu kinachowakwamisha katika matumizi ya kidigitali

Wanahabari wenyewe kuamua kubadilisha mitazamo yao na kuona kwa sasa soko limehamia katika digital ivyo kutafuta nyenzo mbali mbali za kuwasaidia katika mabadiliko hayo.

  Serikali kupitia TCRA kuangazia sheria zinazowabana na kuwanyima uhuru  wanahabari katika matumizi ya kidigitali na kupunguza zinazowabana sana wanahabari ili kuwapa uhuru wa kufanya kazi pasi na kuogopa kufungiwa au kunyanganywa vifaa vya kazi.

Endapo sheria zitaangaliwa na wanahabari kwa ujumla kubadilisha mitazamo yao juu ya matumizi ya kidigitaliwanahabari nchini Tanzania wataweza kunufaika na uandishi wa habari wa kidigitali.

GLORY PASCHAL

DIGITAL JOURNALIST 2021/22

BORESHA HABARI PROJECT

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *