MTANDAO wa kijamii au Mitandao ya kijamii ni Wavuti au huduma ambayo watu huongea,hujumuishwa pamoja na watu wengine  ndani ya nchi ama ulimwenguni kote.  Huduma ya mitandao ya kijamii inaweza kuunganisha watu wenye shauku/mapenzi ya aina moja (kama vile mpira wa miguu shule, ndondi, vyakula vya aina mbalimbali ,filamu dini na kadhalika) pamoja na urafiki.

Sehemu kubwa ya mitandao ya kijamii inakupa fursa ya kutengeneza taarifa zako katika ukurasa wako ikiwa ni pamoja na picha na maelezo kiasi kuhusu wewe mwenyewe, hasa yale ya msingi: unaishi wapi, una asili ya wapi, elimu unapenda nini na kadhalika. Mitandao ya kijamii ilianza kupendekeza tangu hatua za awali za uvumbuzi wa wavuti wa Ulimwengu kwenye  mwaka 1993 Baadhi ya mitandao ya kijamii ambayo ni maarufu sana ni pamoja na Facebook na Twitter inasaidia kuongeza kasi ya mawasiliano  ulimwenguni.

Hata matumizi ya simu ya mkononi zimeanza kupungua umaarufu wake hasa kwa mtindo wa uharaka wake wa kupeana jumbe kupitia mitandao hiyo. Mitandao ya kijamii inatumika kuwaleta watu pamoja na kujenga urafiki miongoni mwao kwani Mitandao ya kijamii inatumika kupeana taarifa na watu wengine.

 Matumizi zaidi ya mitandao ya kijamii yanaendelea kuvumbuliwa katika nyanja tofauti ikiwemo elimu, biashara, matangazo ya kibiashara, siasa,ajira, afya na matibabu, utawalana kadhalika. Mitandao mingi ya kijamii inapatikana katika simu za mikononi hasa zile simu Janja Kuna baadhi ya makampuni yanafungia uwezo wa kuingia katika mitandao ya kijamii hasa kwa malalamiko ya kwamba waajiriwa wanapoteza muda mwingi katika mitandao hiyo.

Hapa tunakutana na Katibu wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma Ben Bago anabainisha kwamba  Changamoto katika vyombo vya habari ni fursa kwa waandishi wa habari wamitandao ya kijamii kwani mitandao ya kijamii imekuja kusaidia jamii kupata taarifa mbalimbali kwa haraka zaidi .

Anasema awali jamii hasa watu wa mikoani walikuwa wakitumia sana magazeti kupata taarifa na ni ukweli kwamba  habari zilikuwa haziwafikii kwa wakati.

” Kunawakati  magazeti yalikuwa yakichelewa  habari ya leo tunaisoma kesho wengi walikuwa wakichelewa kupata taarifa lakini hivi  sasa mitandao imekuja kurabisisha mambo watu wanasoma wanapata matukio mbalimbali kupita  mitandao ya kijamii  kwenye simujanja jambo ambalo ni fursa kwa waandishi wa habari,” amesema Katibu .

Alienda mbali zaidi na kusema” Hata katika kipindi cha Ugonjwa wa UVIKO 19 Mitandao ya kijamii ilikuwa msaada mkubwa kwani watu walikuwa wanawasiliana kwa njia ya Zoom meeting  na kazi zilikuwa zikienda bila kusimama,” amesema Bago.

Naye Asha Mwakyonde mwandishi wa habari wa Blog wa Habari Mateo amesema kuwa mitandao ya kijamii imekuja kurahisisha  kazi hasa kwa waandishi wa habari.

” Mimi zamani nilikuwa naandikia gazeti la Tanzania Daima na ilikuwa unafanya kazi leo unatuma kwa wahariri na habari inatoka kesho lakini sasa kupitia mitandao ya jamii mtu anapata taarifa muda huo huo,” amesema Mwakyonde

https://www.matukiodaimamedia.co.tz/2022/02/fahamu-mitandao-ya-kijamii.html

IMEANDIKWA NA HAMIDA RAMADHANI

MWANDISHI | MATUKIO DAIMA

MWANDISHI WA KIDIJITALI 2021/22

BORESHA HABARI PROJECT

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *