Tunapozungumzia ulimwengu wa kidigitali tuna maana ya kwenda na wakati uliopo na kukabiliana na namna ya kukabikiana na changamoto Ulimwengu wa kidigitali umerahisisha maisha hasa wa kwa wanahabari kwani kwa kugumia simu yako ya mkononi, au computer mpakato (laptop)unaweza kujiajiri kwa kutoa habari mbalimbali kupitia mitandao.
Hii ni kutokana na uwepo  wa teknologia uliorahisisha habari kufika kwa watu kiurahisi mtu anaweza asisikilize redio, asitizame televishen lakini kwa kupitia simu yake akapata habari zote na hapo ndipo dhana ya kuishi kijanja kidigitali inapofanya kazi. Kwetu waandishi wa habari njia hii pia imekua rahisi na ya uhakika kufikisha habari , wengi wetu tunapokua field tunauwezo wa kutoa taarifa (update)ya kile kinachofanyika mahali ulipo kupitia simu janja zetu. Kuishi kijanja kidigitali kumetoa ajira kwa vijana wengi (onlinemedia)kwani kupitia kutoa habari kupitia mitandao mbalimbali mfano kwetu Tanzania kupitia kurasa za jnstagram, youtube, facebook, linkein na mingineyo imewafanya vijana wengi kupata ajira kwa kupokea matangazo na hivyo kuongeza kipato cha kila siku
Kwa maana hiyo ya dhana ya kuishi kijanja kidigitali imefanya wengi wetu kujiajiri na hata kua vyanzo vya kuaminika kwa kuwapasha watu habari . Kama waandishi ni wajibu wetu kuhakikisha tunakimbizana na kasi ya mabadiliko yaani teknologia ili kuhakikisha tunakua wajanja , werevu na hata kufikisha habari kwa uhakika na kwa wakati . Pamoja na uwepo wa changamoto mbalimbali zinazokuepo mfano kukosekana kwa data (vifurushi), internet au mtandao muda mwingine kutokupatikana eneo husika kusifufanye kutokimbizana au kutokuishi kidigitali
Sisi kama waandishi ndiyo watu wa kwanza kuleta mabadiliko kwenye jamii kwa kufikisha habari zenye uhakika
Na kwa vile dunia ipo huko basi tukimbizane na kasi hiyo ili kuwa waandishi wa kijanja na tuishi kidigitali
IMEANDIKWA NA JAMILLA KASSIM | ARUSHAONEFM
MWANDISHI WA KIDIJITALI 2021/22
BORESHA HABARI PROJECT

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *