Miongoni mwa mambo yanayoweza kumtoa mwandishi wa habari kutoka hatua moja kwenda nyingine katika masuala ya kiuchumi ni kujikita katika masuala ya kidigitali. Katika ulimwengu huu wa kidigitali kuna vifaa muhimu ambavyo mwandishi anapaswa kuwa  navyo ili kumsaidia ikiwemo  akaunti za Mitandao ya kijamii.

Hatua hii humfanya mwandishi kuwa na Ujuzi wa kutengeneza  Vitu vingi vinavyoweza kumfanya akaweka habari zenye maudhui fulani kwenye majukwaa yake ya kidigitali,baadhi ya mitandao hiyo ni pamoja na,

1.BLOGU.

Hiki ni kitu muhimu Sana ambacho mwandishi anayeishi kwenye ulimwengu wa Kidigitali anapaswa kuwa nacho,hiki sio tu kinasaidia kusambaza kazi zako bali pia kuzitunza kwa muda mrefu sana na ubora wa blogu ni kuwa unakuwa unaimiliki wewe kama wewe, siyo kama akaunti za mitandao ya kijamii ambazo wamiliki wake ni wenye mitandao hiyo na wanaweza kukufungia mitandao hiyo muda wowote au hata kukuzuia kufanya baadhi ya vitu. Hivyo, kwa sisi waandishi wa habari  tunaoishi kwenye ulimwengu wa kidigititali ni wajibu wetu kuhakikisha tunamiliki blogu zetu kurahisisha mawasilino kwa jamii.

Unaweza kuona kuwa kuweka status za WhatsApp ni sawa, ila ukweli ni kuwa status hizo zinapotea kila baada ya saa 24. Hivyo, nguvu kubwa unayoiweka kwenye kazi yako, inapotea kila baada ya saa 24. ila kwenye blogu haupotezi kitu.

2. SIMU AU KOMPYUTA.

Mwandishi wa Kidigitali anapaswa kuwa na simu au kompyuta au vyote viwili. Hii haimaanishi kwamba usipokuwa na hivi vitu huwezi kuandika, la hasha! Bado unaweza kuandika vizuri tu ila simu au kompyuta inakusaidia kufanya hivyo kirahisi zaidi ikiwa ni pamoja na kusaidia kusambaza kazi zako kwa haraka.

3. BARUA PEPE

Ni wazi kuwa kama mwandishi atakuwa anawasiliana na kushirikiana na wengine kwenye uandishi wake hata hivyo Unahitaji kuwa na baruapepe rasmi ambayo unaitumia kuwasiliana na watu linapokuja suala la uandishi. Mwandishi wa makala haya amezungumza na baadhi ya waandishi mkoani Dodoma ambao wengi wamesema kuna kipindi wanapaswa kutuma kazi zao za kibunifu kwa wahariri, wachapaji au wachapishaji au hata waandishi wengine kwa kuzingatia umakini na umahiri.

Dotto Kwilasa anaeleza kuwa yeye binafsi katika ulimwengu huu wa kidigitali hupendelea zaidi kutumia kazi zake kwa WhatsApp,badala ya kutumia kazi hiyo kwa email .”Siku zote huwa nahakikisha nakuwa makini kusubiri kuona watu wananijibu wakiipokea ili kuthibitisha kuwa wameipokea na hii hunisaidia kwa ajili ya kutunza kumbukumbu za muda mfupi na muda mrefu pia,”anasema.

Hata hivyo anasisitiza kuwa kuna apps nyingi ambazo zinasaidia kutunza kumbukumbu Kidigitali na kukuwezesha kuzipakua muda wowote na sehemu yoyote. Anaeleza kuwa hii ni muhimu sana kwa kila mwandishi maana inawezesha kupata kazi nyingi popote unapokuwa duniani lakini pia inakupa uhakika kuwa hata kama vifaa vyako vya simu au kompyuta vikizima, bado kunakuwa na uwezo wa kupata kazi zako ulizozitunza kimtandao.

“Apps za aina Hii zipo nyingi kama Dropbox, Google documents, Google drive na nyinginezo nyingi,binafsi nazitumia hizo mbili za mwisho na hasa Google document,Email pia inasaidia kutunza kazi Kidigitali.

Hiyo ni baadhi tu mitandao na matumi,I yake hivyo basi kupitia matumizi ya majukwaa ya kidigitali mwandishi anaweza kutengeneza fursa mbalimbali ambazo zinaweza msaidia mwandishi kuingiza kipato. Hii inalenga kuweka maudhui ambayo hutoa elimu na kuhamasisha matumizi salama na sahihi ya mitandao ya kijamii kila mara. Ili kumwezesha mwandishi kutambua jinsi ya kunufaika kiuchumi katika ulimwengu wa kidigitali Tech & Media Convergency kwashirikiana na Internews Tanzania waliendesha mafanzo kwa waandishi wa habari wanawake kwa programu ya Ujuzi wa kidigitali.

Lengo la programu hii ni kuandaa waandishi wa habari wanawake vijana na wale wanaotamani kuwa mmoja wa kuufahamu zaidi kuhusu Ujuzi wa kidigitali, Sheria za Msingi na kanuni zinazoathiri mtandao, kushughulika na kushinda mtandaoni kulingana na jinsi vurugu zinazotokana na mitandao. Programu hii imemfanya mwandishi kutambua kuhusu ujuzi tofauti wa kidigitali na jinsi unavyosaidia katika maendeleo katika ngazi ya kibinafsi na ukuaji wa taaluma kwa ujumla.

Ambapo Mwandishi akiwa na majukwaa ya kidigitali mbalimbali kama youtube au blog anayomiliki mwenyewe  anauwezo wa kuweka maudhui mbalimbali ambayo yanaweza kuelimisha au kuburudisha na kufanya kuwa na wafuasi wengi yaani watazamaji au wasomaji  hivyo kwanjia hiyo anaweza kupata matangazo kutoka,taasisi,mashirika na kampuni mbalimbali mfano makampuni ya simu au asasi zinazojishughulisha na masuala fulani na kupitia matangazo hayo ataingiza kipato kama malipo ya matangazo hayo.

Vilevile mwandishi anaweza kunufaika kiuchumi katika ulimwengu wa kidigitali kupitia maudhui anayoweka kwenye mitandao yake kugusa jamii fulani mfano habari za watoto hivyo ni rahisi kupata madhamini kutoka katika mashirika yanayojishughulisha na masuala ya watoto hivyo husaidia kuendesha vipindi hivyo katika mitandao yako hasa ya video na kuweza kumudu gharama za bando. Kwa maana hiyo mwandishi anaweza kunufaika kiuchumi katika ulimwengu wa kidijitali.

Imeandikwa na Zena Mohamed

Mwandishi | Majira

Mwandishi Wa Kidijitali 2021/22

Boresha Habari Project

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *