Ulimwengu umeingia katika mfumo wa teknolojia iliyokuwa ,hivyo kupelekea kuachana na mfumo wa analojia na kwenda na dijital hii ina rahisisha namana nzuri ya mawasiliano,pamoja na upatikanaji wa taarifa  mbalimabali ndani na nje ya nchi,pia ni mabadiliko ambayo yanaendana  sambamba na ubunifu wa kidijital

Ujuzi wa kidigitali ni uwezo wa kutumia mbinu mpya za kiteknolojia katika kutatua matatizo ya kiutendaji katika  nafasi za uandishi wa habari na kupata matokeo chanya yanayomfanya kutambulika katika ulimwengu wa digitali.

Asha D. Abinallah ambaye ni kiongozi wa kampuni  ya Tech & Media Convergency inayotoa mafunzo kwa waandishi wa habari wanawake kuhusu uandishi wa kidigitali ikiwa na lengo la kuwaendeleza waandishi  wa habari katika uandishi wa habari kutumia teknolojia iliyokuwa.

Amesema  kupitia program hiyo maalumu ya mafunzo ya ujuzi kidigitali inawapa waandishi kupata uelewa na ujuzi wa namna ya kuandaa na kutengeneza maudhui kwa ajili  ya kuyatumia katika majukwaa ya kidijitali.

Abinallah ameongeza kuwa  kutumia  mitandao hiyo kama majukwaa ya uandishi wa habari kwa kuandaa vipindi, habari, makala wanavyoandaa  inasaidia kutengeneza fursa za kujiongezea kipato.

Lilian Urio ni mwandishi wa  kidigitali ambaye pia ni mkufunzi wa mafunzo ya uandishi wa kiditali, amesema  mwandishi  wa habari anapaswa  kujua stadi za kiditali ambazo ndio mwongozo katika kuandaa maudhui pamoja na kujua namna ya kutumia  majukwaa ya digitali.

“Ili kuweza kupata  habari na data kwa usahihi, ili kuandaa maudhui bora  na inayoeleweka kwa jamii ni lazima mwandishi ukubali kubadilika na uendane na kasi ya kukumbatia  huu ujuzi wa kidijitali.” amesema Lilian Urio.

Naye Peter Helatano mwandishi wa habari anaye wakilisha Global tv online Mkoani Rukwa ,amesema ifike mahali waandishi wa habari waone umuhimu wa kukumbatia ujuzu huu wa dijitali kwa kuwa kunafursa nyingi  kwa mwanahabari ambazo zitawaongezea ujuzi,,amesema kupitia simu janja anayotumia inaweza kufanya vitu vingi sana amesema ndio ofisi yake  anayotumia kupata habari,na kutuma habari anazoandaa.

Hata hivyo mwandishi wa habari wa kidigital ni vyema akazingatia kazi za kidijitali ambazo zitamsaidia kuandaa maudhui ikiwa ni pamoja na kujua nanma nzuri ya kutumia mitandao  ya kijamii kukusanya data pamoja na kupata uhakika wa kuandaa maudhui bora kwa kutumia umakini mzuri.

Kupitia uandishi wa habari wa kidigitali kuna faida mbalimbali mwandishi anaweza kuzipata  ikiwa ni pamoja na kujiongezea kipato na kuongeza mawazo mapya ya habari kupitia waandishi wengine,na kuongeza ujuzi katika  kazi yako ya uandishi wa habari ikiwa nipamoja na kujifunza namna watu wanavyo andika habari au kutangaza habari.

ANNA   MALISA | NDINGALA FM 

DIGITAL JOURNALISTS 2021/22

BORESHA HABARI PROJECT

 

 

 

 

 

 

 

 

 

ANNA  MALISA

DIGITAL JOURNALIST 2021/22

BORESHA HABARI PROJECT

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *