Ulimwengu wa Sasa unakua KWA Kasi Sana kutokana na maendeo ya sayansi na teknolojia Katika karne hii 21, na ILI kuendana na kasi hii ya kukua KWA sayansi na technolojia imelazimu watu wa sekta mbalimbali kuona fursa iliyopo na namna ya kutoa huduma zao kidigitali.

Hatua hii ni Katika kurahisisha, utoaji wa huduma KWA wateja, wao, kurahisisha mawasiliano na hata utoaji wa Taarifa za msingi Kulingana na huduma husika.

Fursa ya kutumia njia za kidijital kuifikia Jamii inayohudumiwa inawalenga pia waandishi wa Habari, kutokana na idadi kubwa ya watu wengi kutumia majukwaa ya kidijital kupata taarifa mbalimbali.

Lakini si kila taarifa inayotolewa kupitia majukwaa ya kidijitali imezingatia maadili ya taaluma ya uandishi, nyingi ni taarifa zisizo sahihi KWA sababu wimbi la watoa taarifa ni kubwa tena wale wasio na taaluma, kutokana na hili ndipo Umuhimu wa waandishi wa Habari kujikita kutumia njia za kiditali kuihudumia Jamii unapooneka.

Waandishi wa habari wana mchango mkubwa sana Katika Jamii  iwe nikuhabarisha Umma lakini pia kuelimisha, lakini Kukosa maarifa ya namna ya kutumia njia za kidigitali imekuwa changamoto kubwa ya wao kutojikita Katika uandishi wa Habari kidijitali.

Baadhi ya Waandishi waliozungumza na mwandishi wamesema changamoto kubwa ya matumizi hafifu ya kutumia majukwaa ya kidigitali ni kutokana na Kukosa maarifa ya namna ya kutumia majukwaa hayo kihabari.

Hii ni changamoto iliyoonwa pia na mtandao wa Women at Web na kuamua kutoa mafunzo ya kuwasaidia waandishi wa Habari kujikita Katika uandishi wa kidigitali ILI kuendana na Kasi ya utandawazi uliopo.

Mmoja Kati wa wawezaji wa mafunzo hayo  yaliyoandaliwa na mtandao wa Women @Web, Lilian Urio Ambaye ni Mtayarishaji na mtengenezaji wa maudhui amesema “ni lazima KILA mwandishi ajitafakari mimi kidigitali ni nani, je natumia mitandao ya kijamii? Kama natumia je dhumuni la kutumia mitandao hiyo ni nini, je Chapa au utambulisho wangu Kwenye mitandao ya kijamii kikazi na kitaaluma upoje? Je ninawafikiaje walengwa wangu na je usambazaji wa KAZI ninazozifanya Kama mwandishi wa Habari upoje?”Alisema Lilian.

Hata hivyo Lilian Urio Alitoa muongozo ambao waandishi wa Habari wanapaswa kuzingatia ILI kuwa waandishi wazuri wa kidigitali kwanza ni lazima ajue na kufuata misingi ya uandishi wa Habari kidigitali ikiwa ni pamoja na kuongeza ujuzi na maarifa ya namna ya kutumia majukwaa hayo ya kidigitali, uelewa mzuri wa lugha anayopaswa kuitumia, uwezo wa kuthibitisha na kuchunguza taarifa KWA usahihi, kujua kanuni za mahojiano pamoja na uwezo wa kufikiria na umakinifu.

Vilevile akaongeza kuwa Ubunifu wa kidijital ni  Jambo la muhimu pia ili kutumia mbinu za kitecknolojia Katika kuwafikia unaowahudumia na kutatua changamoto mbalimbali ILI kupata matokeo chanya na ya kipekee uliyoyahitaji.

Uandishi wa Habari kidijitali humsaidia mwandishi kujijengea chapa binafsi (brand), kufikisha habari zake KWA watu wengi zaidi KWA muda mfupi pamoja na  kutumia majukwaa hayo Kama sehemu ya kujiingizia kipato.

IMEANDIKWA NA ELIZABETH TANZANIA

MWANDISHI WA KIDIJITALI 2021/22

BORESHA HABARI PROJECT

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *