
KUWA mwandishi wa habari, mara nyingi, ni taaluma ya ufundi na Teknolojia mpya zinazowakilisha mabadiliko katika ulimwengu wa uandishi wa Habari na kutoa fursa mpya za ukuaji wa kazi zao.Kwa upande mwingine, uandishi wa habari wa kidijitali au teknolojia unahusishwa kikamilifu na mambo ya sasa kwani unatoa jibu kwa upesi kwa wadau wa Habari ambapo wanadai wanapotaka habari kupitia data iliyothibitishwa basi inapatikana kiurahisi.
Akiongea na Uhuru digital na uhuru Gazeti Mkurugenzi Mkuu wa Media Convergency Asha Abinallah anasema kuwa ili Kuendana na wakati wa sasa wa teknolojia ,Wanahabari nchini wanapaswa kuhakikisha wanabadili uandishi wao waliouzoea na badala yake waendane na uandishi wa Habari wa kidijitali ambao ndiyo uko kwenye soko la ulimwenguni wa sasa.
Anasema Kazi ya mwandishi wa habari wa digital ni muhimu sana leo,kwani hukuza dhamira yake kwa maadili ya kitaaluma, hutafuta ukweli na hutofautisha habari.
“Kwa njia hii, inatoa ubora na maudhui ya ubunifu na Kupitia mafunzo maalum na uzoefu wa mikono, mwandishi huongeza hali yake ya kibinafsi,kwani kwa njia hii lazima kazi yake inatofautiana na ile iliyofanywa na wataalam wengine ambao hayuko kidijitali.
Asha anasema kwa kutumia uandishi wa kidijitali , wasomaji watakuwa na fursa ya kufurahia maudhui ya ubora katika vyombo vya habari tofauti kama kwenye magazeti,vituo vya television,blog ,radio, onlines na mitandao ya kijamii.
“Utaona hata kiwango cha kufikia habari zinazosimuliwa kupitia gazeti la kidijitali, jarida au blogu ni cha juu. na wasomaji kutoka sehemu mbalimbali za dunia wanaweza kupata chanzo kimoja”anasema.
Hivyo Asha anasema wanahabari wanapaswa kuwa wa kidijitali ili kupambanua uandishi wao na siyo wa onlines pekeyao bali hata wengine kupitia vyombo vyao vya Habari wataweza kuwa waandishi wa kisasa kwa kutumia mitandao ya kijamii kupata Habari au fulsa mbalimbali katika mashirika au taasisi za kijamii.
“Mwandishi ambaye bado anatumia njia za zamani au uandishi wa zamani katika kufanya kazi zake basi hata Habari yake haikidhi matarajio ya msomaji ,msikilizaji hata mtazamaji”anasema.
Uandishi wa karne ya 21 unakuja kwa kuendana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia yanayoendana na karne hiyo,hivyo kwa mwandishi kushindwa kuendana na kasi ya kidijitali basi hata mtazamo wa ubunifu hufanya maudhui kuwa ya kawaida na yasiyovutia.
Nae Meneja Mawasailano Women In News Tanzania Yvonne Kigano anasema waandishi hapa nchini Tanzania hawana budi kufanya kazi zao kwa kutumia mfumo wa kidijitali yanayoendelea kutokea duniani, ikiwemo kuibuka kwa mitandao ya kijamii na fursa zinazoambata na mabadiliko hayo.
Yvonne anasema Mitandao ya kijamii ni kipaza sauti kizuri kwa wale wataalamu wanaofanya kazi katika uwanja huu na kupitia chaneli wanaweza kueneza kazi zao na umma ukazipata kazi . Anasema waandishi walio wengi wamekuwa wakitumia uandishi wa zamani na matokeo yake uandishi wao unakuwa ni uleule ambao haumvutii msomaji wala mtazamaji sababu alichoandika hakimlengi msomaji na hauko katika mpangilio ulio mzuri .
“Wito wangu kwa wanahabari kuangalia nyakati za sasa za kidijitali zinazomtaka mwandishi kumlisha msomaji wake kupitia maudhui ya digital na kutambua kuwa Mitandao ya kijamii haitoi tu fursa mpya za kitaaluma kwa waandishi wa habari bali pia inaleta maendeleo ya tabia mpya kwa wasomaji ambao, leo, wanasom,wanasikilia na kutazama habari kupitia simu za mkononi.
Wakiongea na Uhuru Digital na Uhuru gazeti kwa nyakati tofauti walisema uandishi wakidijitali ni muhimu kwa wanahabari kwa karne hii ya 21,kwani jamii inadai habari ya kisasa kuhusiana na habari zinazochipuka na matukio hasa katika mitandao ya kijamii.
“Kazi ya mwandishi wa habari wa digital ni muhimu sana leo, sababu inakuza dhamira yake kwa maadili ya kitaaluma na hutafuta ukweli sanjali na kutofautisha Habari”,anasema Haika Sanga wa Clouds TV Mkoa wa Songwe.
Aidha Haika anaongeza kuwa uandishi wa kidijitali kupitia Mitandao ya kijamii husaidia kukusanya Habari mbalimbali na kuzifanyia kazi lakini pia kupata wazo la kesho la kulifanyia kazi,Pamoja na hayo pia uandishi wa kidijitali unamsaidia mwandishi kujua vitu mbalimbali na mifumo mbalimbali ya kuitumia anapofanya kazi yake ya kihabari.
Kwa upande wake Dickson Kapungu wa Global Tv Songwe,anasema kuwa Uandishi wa kidijitali nimuhimu sana kwa wakati wasasa kwani inatoa ubora na maudhui ya ubunifu,hivyo elimu na mafunzo mbalimbali yanahitajika zaidi ili kubadilisha mtazamo wa wanahabari na matumizi ya mitandao ya kijamii.
Kapungu anasema kupitia mafunzo maalum watakayopewa na uzoefu wa mikono yao, mwandishi ataweza kuongeza hadhi yake na kazi yake itaonekana bora na kuliko anayetumia mfumo wa zamani katika uadishi wake,hivyo uandishi wa habari wa kidijitali kwa sasa unatoa kiwango cha juu cha kuajiriwa.
IMEANDIKWA NA ANITA BOMA
MWANDISHI | UHURU MEDIA GROUP
MWANDISHI WA KIDIJITALI 2021/22
BORESHA HABARI PROJECT