Wakati dunia ikikuwa kwa kasi na mambo yakibadilika kila uchwao waandishi wanawake wamehimizwa kujikita katika kutumia mbinu za kisasa katika kazi zao za uandishi ili kuendana na kasi hiyo

Hayo yamejiri katika mafunzo ya digital skills yaliyotolewa na shirika la WOMEN AT WEB TANZANIA  na kuendeshwa kwa njia ya mtandao(online)  na mkufunzi LILY URIO,amesema hivi sasa tupo katika kipindi ambacho dunia inapitia teknolojia kubwa na za kisasa  pamoja na matumizi ya simu janja ,kuenea kwa mitandao ya kijamii ,internet za kasi ya 3G na 4G zimerahisisha dunia katika kusafirisha Habari kwa haraka  ikiwa ni Pamoja na utendaji kazi mbalimbali katika jamii lakini pia kushirikishana katika fursa mbalimbali ambazo zimeibuka kutokana na teknolojia  kukua

Amesema kuwa waandishi wa Habari wanawake wanaweza kufungua chaneli zao kama vile instagram, facebook, Telegram, youtube binafsi mtandaoni na kuanza kuweka maudhui yatakayoelimisha jamii ikiwa kuandika simulizi za kidigitali   kutengeneza Makala mbalimbali na kuandika Habari au kuweka biashara zao mtandaoni ili kuweza kujipatia kipato

Akizungumzia manufaa ya mitandao ya kijamii  mkufunzi huyo amesema waandishi wa Habari hasa wanawake wakiitumia vizuri mitandao ya kijamii itawafanya wafahamike kwa haraka katika jamii na mwisho wa siku kuweza kujipatia kipato kwa sababau tayari watakuwa wamejitengenezea jina

‘’Mitandao ya kijamii ni njia nzuri sana pale itakapotumiwa vizuri na waandishi kutokuogopa kuthubutu kufanya jambo ambalo mbeleni litaleta manufaa katika Maisha yao kuna watu wanalia na changamoto ya vifaa kama laptop hapana unaweza fanyia kazi zako za kuchapisha habari  hata  kwa kutumia simu janja mwisho wa siku utaona faida yake amesema mkufunzi Lilly

Glory Paschal  mwandishi wa habari wa kituo cha  redio uvinza  mkoani Kigoma ni miongoni mwa watu waliopata mafunzo hayo amesema  mafunzo   aliyoyapata atayatumia kwa kuanza kuyafanyiakazi;

‘’Ili kuendana na kasi ya teknolojia na inavyokuwa inabidi nianze kuchapisha Habari zangu katika mitandao ya kijamii japo zinasikika redioni lakini sasa ninayo haja ya kufungua kurasa zangu za mitandao ya kijamii na kuanza kuzipeleka huko kazi zangu ili watu mbalimbali waweze kuzisoma’’ Amesema Glory

EDITHA EDWARD | UVINZA FM

DIGITAL JOURNALISTS 2021/22

BORESHA HABARI PROJECT

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *